Uchaguzi: Chama cha ANC chakabiliwa na upinzani mkali Afrika Kusini

Raia wa Afrika kusini wapiga foleni kuwachagua viongozi wa mabaraza nchini Afrika Kusini
Image caption Raia wa Afrika kusini wapiga foleni kuwachagua viongozi wa mabaraza nchini Afrika Kusini

Watu nchini Afrika Kusini wanapiga kura za kikanda ambazo zinaonekana kuwa kipimo cha umaarufu wa chama cha African National Congress na rais Jacob Zuma.

Kura ya maoni inaonyesha kuwa ANC inakabiliwa na upinzani mkali kwa mara ya kwanza tangu kumalizika kwa utawala wa ubaguzi wa rangi katika miji mikubwa kama Pretoria, Johannesburg na Port Elizabeth.

Ukosefu mkubwa wa ajira na sakata za ufisadi vimeathiri umaarufu wa ANC na kusababisha kuinuka kwa vyama vya upinzani.