Utafiti:Papa wa Greenland wanaishi kwa muda mrefu zaidi

Image caption Papa wa Greenland akielea katika maji baada ya kufanyiwa utafiti

Utafiti mpya unaonesha papa wa Greenland ndio papa wanaishi kwa muda mrefu zaidi kuliko viumbe wote wenye uti wa mgongo, wanaishi hadi miaka 400. Wanasayansi wamefanya uchunguzi wa kina kujua wanaishi umri gani na wamegundua papa hao wanaishi muda mrefu kuliko viumbe wengi wa baharini.

Image caption Papa wanaishi kwa muda mrefu zaidi kuliko viumbe wote wenye uti wa mgongo

Papa wa kike huchelewa kukomaa na kuzaa hadi kuanzia miaka 150. Inasemekana asili yao ni kukua taratibu. Papa hao wana uwezo wa kufikia urefu wa mita 5.