Waliowaua raia 10 wa Ethiopia washtakiwa

Zaidi ya wasudan 270,000 wanaishi Gambella nchini Ethiopia.
Image caption Zaidi ya wasudan 270,000 wanaishi Gambella nchini Ethiopia.

Wakimbizi kutoka nchini Sudan Kusini walio katika taifa jirani wa Ethiopia wamefunguliwa mashtaka baada ya kuwaua watu 10 raia wa Ethiopia.

Watu hao 23 wanaripotiwa kutekeleza mauaji hayo kwenye kambi moja ya wakimbizi, iliyo mkoa wa magharibi mwa Ethiopia wa Gambella mwezi Aprili, kulipiza kisasi ajali ya gari ambapo watoto wawali wakimbizi waliaga dunia.

Taarifa za mahakama zinasema kuwa mauaji hyao yalipangwa na wanawake wawili ni kati ya wale waliouawa.

Zaidi watu 270,000 raia wa Sudan wanaishi kama wakimbizi katika mkoa wa Gambella, baada ya kukimbia ghasia ambazo zimeikumba nchi yao tangu ipate uhuru mwaka 2011.

Mada zinazohusiana