Harusi za usiku zapigwa marufuku Mombasa

Sherehe za usiku Haki miliki ya picha AFP
Image caption Sherehe za usiku

Mamlaka katika mji wa pwani ya Kenya, Mombasa imepiga marufuku harusi za usiku kutokana na sababu za kiusalama.

Kamishna wa eneo hilo Maalim Mohammed anasema kuwa hatua hiyo inalenga kuwalinda wakaazi dhidi ya mashambulio ya magenge yanayotumia visu.

Magenge hayo yamekuwa tatizo kubwa kwa wakaazi katika siku za hivi karibuni huku baadhi ya wakaazi wakiripoti kushambuliwa wakati wa mchana .

Maafisa wa polisi wamekuwa wakifanya operesheni za kiusalama huku washukiwa kadhaa wa magenge hayo wakiuawa.

Wakaazi wa pwani hufanya sana harusi za usiku ambazo huendelea kwa takriban siku kadhaa ikiwemo sherehe za usiku.

Mada zinazohusiana