Mgomo wasababisha maduka kufungwa DRC

Maduka yaliofungwa mjini Kinsasha
Image caption Maduka yaliofungwa mjini Kinsasha

Wamiliki wa maduka walisalia majumbani mwao nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wakati wa mgomo wa upinzani mjini Kinshasa.

Mgomo huo wa kitaifa uliitishwa na upinzani kuhusu madai ya jaribio la kusongesha mbele tarehe ya uchaguzi wa urais unaotarajiwa kufanyika mwezi Novemba ,pamoja na kuachiliwa huru kwa wafungwa wote wa kisiasa.

Hapo jana rais Kabila aliwaachilia huru wafungwa 24.

Image caption Maduka yaliofungwa mjini Kinsasha

Lakini kulingana na BBC Afrique,upinzani na unadai kwamba idadi hiyo ni ndogo mno.

Vyama vikuu vya upinzani nchini humo MLC na UDPS ambavyo vinasusia mazungumzo ya kitaifa vimepinga hatua hiyo vikisema vinataka zaidi ya wafungwa 100 wa kisiasa kuwachiliwa huru.