Marekani yapokea mkimbizi toka Syria

wakimbizi Haki miliki ya picha AP
Image caption Wakimbizi wakiokolewa

Utawala wa Rais Barack Obama umesema umepokea mkimbizi wa Syria aliyefikisha idadi ya wakimbizi wa Syria waliopokewa na Marekani kuwa jumla ya wakimbizi 10,000. Mwezi Septemba mwaka uliopita Rais Obama aliahidi kuwakaribisha wakimbizi elfu kumi wa Syria hasa wanaokabiliwa na tisho la kuangamizwa. Ikulu ya Marekani imepongeza hatua ya sasa na kusema imeafikiwa mwezi mmoja kabla ya ilivyotarajiwa.

Mkuu wa idara ya polisi nchini Mexico, Enrique Galindo, amefutwa kazi, baada ya ripoti ya tume ya taifa ya haki za binadamu kudai kwamba polisi waliwaua kwa makusudi washukiwa na genge la ulanguzi wa mihadarati. Rais wa Mexico amemuachisha kazi bwana Galindo ili kutoa nafasi ya uchunguzi huru kufanywa.

Rais aliyesimamishwa kazi nchini Brazil Dilma Rouseff, ameambia Baraza la Senate kwamba anawindwa kisiasa na wale ambao aliwashinda katika uchaguzi mkuu miaka miwili iliyopita. Bi Rousseff anahojiwa na Seneta ikiwa ni awamu ya mwisho kuamua ikiwa atasalia madarakani. Kumekua na maandamano kati ya wafuasi na wapinzani wake.