Kandanda kukusanya madawati mwaka huu

madawati Haki miliki ya picha Google
Image caption mpra wa miguu kutumika kuchangia madawati

Tamasha la Kandanda maarufu kama 'Kandanda Day', linatarajia kufanyika Oktoba 15, mwaka huu katika kiwanja cha Jakaya Kikwete Park (zamani Kidongo Chekundu).

Katika tamasha la mwaka huu,kauli mbiu itakuwa ni 'Mpira na Dawati',kwa maana ya tamasha hilo kutumika kukusanya fedha kwa ajili ya kununua madawati yatakayogawiwa kwa shule mbalimbali nchini kutoka na uhaba ulioko Tanzania."Umekuwa ni utaratibu wetu kila mwaka huu,kuja na kauli mbiu ambayo itahusisha soka na jambo ambalo moja kwa moja linaihusu jamii,kwahiyo, tumeona kwa kutumia soka,tunaweza kuisaidia jamii yetu kwa urahisi,"alisema Mkangara na kuongeza:

"Ndio maana kwa miaka yote tuliyofanya tamasha letu,kumekuwepo na mrejesho wa moja kwa moja kwa jamii inayotuzunguka,kwa hiyo ule utamaduni wetu tuliokuwa nao kwa miaka minne tunaendelea nao kwa mwaka huu kwa kukusanya fedha kwa ajili ya manunuzi ya madawati,ambapo tunatarajia kuchangisha fedha na kuuza jezi katika chakula cha hisani kwa wadau mbalimbali."

Mkangara,alisema "Tamasha hili la kila mwaka lina wigo mpana,kutokana na ushiriki wa wadau wa mikoani,hivyo,kwakuwa hili jambo ni la kitaifa,tumeamua kama kamati kugawa madawati kwa wawakilishi wetu wa mikoani ambao tunatarajia watashiriki tamasha letu,huku tukiwaomba wadau wengine watuunge mkono katika kampeni yetu,"alisema Mkangara

Tamasha la mwaka huu linatarajia kushirikisha timu mbalimbali alikwa,ukiacha timu wenyeji Time Dizo Moja na Timu Ismail.Pia,tamasha hilo linatarajiwa kupambwa na burudani mbalimbali na michezo ya kuvuta kamba kwa washiriki.