Vitendo vya kibaguzi vyakemewa Marekani

Afisa mwandamizi wa Umoja wa Mataifa Haki miliki ya picha EPA
Image caption Zeid Ra'ad al-Hussein

Ofisa mwandamizi wa Umoja wa mataifa ameonya juu ya kuendelea kuyapa umaarufu mataifa ya magharibi yanayounga mkono itikadi ya mrengo wa kulia kwamba hali hiyo inaweza kuleta machafuko.Tume ya juu ya umoja wa mataifa ya haki za binadamu imemkemea Donald Trump, na kuishitaki Republican kwa kuendeleza vitendo vya kibaguzi dhidi ya binadamu na chuki za kidini.

Akizungumza mbele ya baraza la ulinzi huko Netherland, Zeid Ra'ad al-Hussein amesema kuwa kiongozi wa mlango wa kulia Geert Wilders amekuwa mmoja viongozi wazalendo wafitini wanaotumia ubaguzi wa rangi kama silaha ya kisiasa.

Pia, alisema Nigel Farage nchini Uingereza na Marine le Pen wa Ufaransa unafanana na wapiganaji wa islamic state ambao wamejenga uoga kama mbinu ya kuhamasisha chuki na vurugu.