Ziara ya Trump Mexico, waziri wa fedha ajiuzulu

Mexico
Image caption Rais wa Mexico Enrique Pena Nieto na mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Republican

Waziri wa Fedha nchini Mexico, Luice Videgaray amejiuzulu wadhifa wake wiki moja baada ya ziara yenye utata iliyofanywa na mgombea Urais wa Marekani Donald Trump. Kwa kiasi kikubwa inaonekana kuwa Videgaray ndiye mwanasiasa aliyepanga ziara hiyo iliyomkutanisha Trump na rais wa nchi hiyo Enrique Pena Nieto, jambo liliwakasirisha raia wa Mexico.

Mgombea huyo wa urais kupitia chama cha Republican ameahidi kuwa ikiwa atachaguliwa kuwa rais wa nchi hiyo atajenga ukuta utakaotenganisha mpaka wa Mexico na Marekani ili kuwafanya watu wa Mexico waweze kuulipia.

Nafasi ya Videgaray sasa imeshikiliwa na Jose Antonio Meade, ambaye ni mchumi mzoefu na tayari amejiunga na baraza la mawaziri wakati huu serikali ikijiandaa kubana bajeti.