Marekani yasema, shambulio la New York ni ugaidi

Shambulio la bomu New York Haki miliki ya picha AFP
Image caption Shambulio la bomu New York

Gavana wa New York, Marekani Andrew Cuomo amesema bomu lililolipuka usiku wa Jumamosi mjini New York ni Ugaidi.

Lakini Cuomo amesema halina uhusiano na vikundi vya kimataifa vilivyopatikana.

Meya wa jiji la New York Bill de Blasio, amesema uchunguzi uliofanyika ulijaribu kubaini sababu hasa ya kufanyika shambulio hilo, lililojeruhi watu 29.

Polisi wa ziada elfu moja na walinzi wa taifa wamesambazwa katika jiji hilo kama tahadhari.

FBI wamesema kuwa wachunguzi wanapima mabaki ya bomu na kifaa kingine cha mabomu kilichokutwa hatua nne tu kutoka eneo la mlipuko.