Winnie Mandela aukosoa uongozi wa ANC

Winnie Madikizela Mandela
Image caption Winnie Madikizela Mandela

Winnie Madikizela-Mandela amekosoa vikali uongozi wa chama tawala cha taifa hilo ANC.

Winnie ambaye alikuwa mkewe rais wa zamani wa taifa hilo Nelson Mandela na ambaye alipigana vita dhidi ya ubaguzi wa rangi, ameambia waandishi habari: ''Hatuwezi kujifanya kwamba hakuna matatizo''.

Amesema kuwa kuna vitu vingi ambavyo vimefanywa kimakosa na kwamba chama hicho kinahitaji uongozi mpya ili kushirikiana na viongozi wazee wa chama.

Image caption Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma

Pia amelalamikia kuhusu ufisadi nchini humo na kuongezea kwamba sasa ni wakati wa watu kujichunguza.

Matamshi yake yanajiri wakati ambapo mirengo tofauti ya chama hicho inakabiliana kuhusu kuimarisha uungwaji mkono wa chama hicho baada ya matokeo mabaya ya uchaguzi wa serikali za mitaa.