Mwandishi wa Redio Shabele auawa kwa risasi, Somalia

un Haki miliki ya picha Google
Image caption bendera ya Umoja wa mataifa

Mwandishi mmoja wa habari ameuawa kwa kupigwa risasi mjini Mogadishu nchini Somalia.watu waliokuwa na silaha wakiwa kwenye pikipiki walimpiga risasi Abdi Asis Mohamed Ali alipokuwa akirudi nyumbani kwake.

Abdi Asis alikuwa akifanya kazi kwenye radio moja binafsi iitwayo Shabelle ambayo wafanyakazi wake awali waliwahi kulengwa na mashambulizi

Mwandishi wa habari huyo ambaye amefanya kazi na Radio Shebelle kwa miaka kadhaa alipigwa risasi na watu wawili wenye silaha wakiwa na pikipiki mjini Mogadishu na kupoteza maisha.

Uongozi wa Redio aliyokuwa akifanyia kazi umethibitisha kifo chake na kusema watu wenye silaha walitoweka kwenye eneo la tukio,hii si mara ya kwanza kwa waandishi wa habari wa Redio Shabele kuuawa kwa kupigwa risasi nchini Somalia.

Umoja wa Mataifa hivi karibuni ulitoa ripoti ikiiorodhesha Somalia kuwa miongoni mwa nchi hatari kwa waandishi wa habari kufanya kazi. Ripoti zao zinasema kati ya mwezi agosti mwaka 2012 mpaka june 2016, waandishi wa habari 30 waliuawa nchini Somalia.

Ripoti hiyo inasema karibu waandishi wa habari 120 wamekamatwa na wanashikiliwa kati ya januari mwaka 2014 na Julai mwaka 2016