Mashambulio yasitisha huduma za hospitali Aleppo

Hospitali kuu ya Aleppo yashambuliwa
Image caption Hospitali kuu ya Aleppo yashambuliwa

Madaktari mjini Aleppo nchini Syria wanasema kuwa huduma kwenye hospitali kuu katika eneo linalodhibitiwa na waasi zimesitishwa kabisa na mashambulizi ya ndege.

Daktari mmoja alisema kuwa mabaki ya jengo hilo yana giza na hakuna wahudumu au walinzi waliobaki.

Ndege za Syria na Urusi zimetekeleza mashambulizi makubwa maeneo ya mashariki mwa Aleppo tangu makubaliano ya kusitisha vita ya mwezi uliopita yavunjike.

Image caption Watu 2 waliuawa wakati wa mashambulio hayo ya angani

Mamia ya raia wameuawa na idadi kubwa ya watu kujeruhiwa.

Nchi za Ghuba zimeutaka Umoja wa Mataifa kuingilia kati mara moja ili kusitisha mashambulizi hayo ya angani.