Obama atangaza hali ya hatari Florida kutokana na kimbunga Hurricane Matthew

Obama ameviagiza vikosi vya uokoaji kuwa tiyari wakati wowote
Image caption Obama ameviagiza vikosi vya uokoaji kuwa tiyari wakati wowote

Rais wa Marekani Barrack Obama ametangaza hali ya hatari katika mji wa Florida baada ya picha za Satellite kuonyesha kimbunga Hurricane Matthew kinaelekea eneo hilo.

Vikosi vya uokoaji navyo vimejiandaa kutoa msaada pale inapobidi.

Kwasasa kimbunga Matthew kimesababisha kasi ya upepo kwenda kwa kilomita 220 kwa saa moja.

Image caption Kimbunga Hurricane Matthew

Mamilioni ya watu katika majimbo manne nchini Marekani wamenza kuhama makazi yao hususani aeneo ya mwambao wa pwani ili kuepuka kukumbwa naathari za moja kwa moja za kimbunga hicho.