Sudan yaongeza bei ya mafuta kwa asilimia 30

Sudan imeathiriwa na kushuka kwa bei ya mafuta duniani Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Sudan imeathiriwa na kushuka kwa bei ya mafuta duniani

Serikali ya Sudan imeongeza bei ya mafuta kwa asilimia 30, kutokana na changamoto za kiuchumi zinazolikumba taifa hilo.

Sudan imeathiriwa na bei za chini za mafuta na vikwazo vya kimataifa pamoja na uhuru wa Sudan Kusini, ambapo kuna hifadhi kubwa ya mafuta iliyokuwa ikipiganawa na Sudan

Mara ya mwisho serikali ya Sudan Kusini iliongeza bei ya mafuta, kulitokea maandamano barabarani wakati eneo bei zilipanda kwa asilimia 60.

Miezi ya hivi majuzi Sudan ilikumbwa na uhaba wa mafuta wa ya petrol na diesel.