Trump awapigia simu marais wa Korea Kusini na Japan

Trump azihakikishia uhusiano bora Korea Kusini na Japan Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Trump azihakikishia uhusiano bora Korea Kusini na Japan

Rais mteule nchini Marekani Donald Trump ameihakikishia Korea Kusini kuwa, atadumisha uhusiano mzuri uliopo kati ya Marekani na Korea Kusini, kwa mujibu wa rais wa Korea Kusini Park Geun-hye.

Trump aliahidi wakati ya mawasiliano ya dakika kumi kwa njia ya simu siku ya Jumatano kuwa, nchi hizo zitadumisha ushirikiano uliopo na kujilinda kutokana a na kile alichokitaja kuwa msukosuko uliopo Korea Kaskazini.

Ofisi ya Park ilimnukuu Trump akisema, "tutakuwa nanyi kwa asilimia 100."

Mwezi Machi wakati wa mahojiano na gazei la New York Times, Trump aliilaumu Korea Kusini kwa kukosa kulipia maelfu ya wanajeshi wa Marekani walio nchini humo, na kutishia kuwa anaweza kuwaondoa ikiwa atachaguliwa.

Matamshi yake yalikaribishwa na Korea Kusini wakati huo..

Trump pia alizungumza na waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe, kulingana na maafisa nchini Japan. Msemaji wake alisema kuwa Abe na Trump walizungumzia umuhimu wa ushirikiano kati ya Japan na Marekani ambapo walipanga kukutana baadaye mwezi huu.