Msimu wa Wanawake 100 wa BBC: Utarajie nini?

Alicia Keys Haki miliki ya picha THEO WARGO
Image caption Alicia Keys ni mmoja wa wanawake maarufu wanashiriki katika msimu wetu huu

Msimu wa Wanawake 100 wa BBC umerejea, na mara hii kwa kishindo zaidi!

Kwa wiki tatu zijazo tutakuletea taarifa kuhusu Wanawake 100: msimu wa majadiliano kinzani, midahalo kuhusu kujumuishwa kwa haki za wanawake na mazungumzo na viongozi maarufu katika nyanja za muziki, michezo na siasa, pamoja kauli nyingine za watu ambao hawatambuliki sana.

Haya ni baadhi ya mambo unayopaswa kutarajia:

Mwandishi na mwimbaji w Alicia Keys akizungumza nasi kuhusu asili na rangi, Donald Trump, malezi ya vijana na kwanini ameazimia kuwa na muonekano anaoutaka yeye.

Simone Biles anatueleza kuhusu kuwa mchezaji sarakasi maarufu, kuhusu kukua katika Marekani ya Obama, na kuhusu namna anavyokabiliana na maisha mapya ya umaarufu.

Image caption Wanawake 100: Tamasha ya kwanza Mexico City tarehe 24 Novemba

BBC Wanawake 100 itaandaa tamasha ya kwanza ya moja kwa moja katikati mwa jiji la Mexico City, litakalokuwa na muziki, sanaa, densi na mdahalo.

Tamasha hii ya Mexico pia itaonyesha uzoefu wa shughuli za BBC. Wenye misingi ya ushuhuda kutoka kwa wanawake waliookolewa, kipindi cha televisheni kitakachokuwezesha wewe ''kuishi'' maisha ya mwanamke ambaye alisafirishwa na mtandao wa magenge ya mihadarati ambaye anakaribia kuokolewa.

Tunataka WEWE ushiriki kwa kutoa maoni yako, mitizamo na fikra.

Unaweza kutupata katika: Facebook, Instagram, Twitter, na YouTube.

Watangazie wenzako kwa kuwashirikisha taarifa zako uzipendazo na taarifa zako kupitia kitambulisha mada #100women

Ujasiri

Mwezi Julai mwanamke mwenye umri mdogo wa Kimaarekani aliyekuwa amevalia gauni zuri refu alisimama akiwa amekunja mikono yake kifuani huku akiwatazama askari polisi waliokuwa wamejihami kwa silaha nzito waliokuwa mbele yake.

Mwanamke nyuma yake ambaye kwa sasa ni mpigapicha maarufu, ni Ieshia Evans.

Haki miliki ya picha JONATHAN BACHMAN
Image caption Picha ya Leshia Evans wakati wa maandamano wakati wa majira haya ya kiangazi

Anaongea nasi kuhusu maandamano na upinzani. Ieshia ni mmoja wa wanawake watano katika mfulurizo wa mazungumzo na wanawake watano wanaokaidi matarajio na mipaka kutoka maeneo mbali mbali ya dunia.

Katika mazungumzo maalum, tutaangazia swali muhimu: Je, haki za wanawake zinawajumuisha wanawake wote? Kimberle Williams Crenshaw, Heather Rabbatts na Gail Lewis watabainisha ikiwa vuguvugu la wapigania haki za wanawake limefanikiwa katika kuwashirikisha wanawake wote bila kujali rangi, kabila na msimamo wa mtu kuhusu mapenzi.

Haya ni mazungumzo yatakayokuwa katika sehemu tatu ambayo usingependa kuyakosa.

Mtandao wa BBC Asia pia utashiriki katika msururu wa midahalo, ukiuliza: "Je wanawake Waingereza wenye asili ya Asia wamepiga hatua?" shiriki mazungumzo haya kupitia#100Women.

Wanawake 100 inamaanisha nini?

BBC wanawake 100 majina ya wanawake 100 wenye ushawishi na wa kuigwa kutoka maeneo mbali mbali ya dunia kila mwaka.

Tunabuni vipindi, mahojiano na taarifa zinazowazungumzia kuhusu maisha yao, kutoa zaidi muda kwa taarifa zinazozungumzia wanawake . Tunaendelea kuhoji: :

Wanawake wako wapi kiuchumi katika karne hii ya 21?

Wanawake wanaweza kushikilia wadhfa mkubwa katika siasa na biashara ? Ama kuna uwezekano wa " kuongoza dunia".?

Nini tunazoona kama hatari kubwa wanazokabiliana nazo wanawake zaidi? Wanafursa gani kubwa ?

Na - bila shaka - ni vipi kuhusu vyombo vya habari? Je hatwawakilishi wanawake ? Je tunaeleza taarifa zao ipasavyo?

Tunataka WEWE kushiriki kwa kauli zako, maoni na fikra . Unaweza kutupata katika : Facebook, Instagram, Pinterest, Snapchat, na YouTube.

Toa taarifa hii kwa kushirikisha taarifa uzipendazo na uzoefu wako kupitia #100women

Kutana na Mama wa Miti.

Tunatembelea mwanamke mwenye umri wa miaka 105- Saalumarada Thimmakka ambaye alipanda na kukuza mamia ya miti aina ya banyan trees eneo la vijijini India, kwa lengo la kuboresha mazingira yake na kupambana na unyanyapaa uliozingira maisha yake ya utotoni.

Image caption Saalumarada Thimmakka alikuza mamia ya miti nchini India

Tunakamilisha msimu wetu wa makala haya kwa kuhoji je : Kuna ubaguzi wa jinsia wa mtandao? Wikipedia ni mtandao wa saba kwa umaarufu katika internet duniani lakini 15% ya wahariri wa Wikipedia ni wanawake na chini ya 15% ya wasifu wa watu wake muhimu ni wanawake.

Tunajiunga na Wikipedia katika muda wa saa 12 wa uhariri ili kuwahamasisha wanawake zaidi kuhariri na kuandika taarifa na wasifu juu ya wanawake.

Tarehe 8 Disemba tunataka ushiriki- jiunge na wavuti wetu, ujifunze jinsi ya kuhariri na kujiunga na hashtag #100womenwiki

Mada zinazohusiana