Cameroon: Vikosi vya usalama vyawatawanya waandamanaji wanaopinga kifaransa

Rais wa Cameroon Paul Biya
Image caption Rais wa Cameroon Paul Biya

Nchini Cameroon vikosi vya usalama vimewatawanyisha kwa mabomu ya machozi na risasi waandamanaji waliokuwa wakipinga serikali Kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo.

Inasemekana kuwa baadhi ya watu wamefariki na wengine kujeruhiwa katika mji wa Bamenda.

Maandamano yalianza siku ya Jumatatu wakiwaunga mkono walimu walikokuwa wakipinga kuanzishwa kwa Lugha ya kifaransa mashuleni katika maeneo yanayozungumza Anglofone huko nchini Cameroon.

Wanasheria wamekuwa wakiandamana kwa kipindi cha wiki mbili kufuatia kuamrishwa na Serikali kutumia lugha ya kifaransa katika masuala ya kisheria.

Wacameroon wengi huzungumza lugha ya kifaransa huku watu wa maeneo yanayozungumza kingereza wamesema wanadharaulika