Debuchy nje kwa miezi sita

Beki wa Arsenal Mathieu Debuchy Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Beki wa Arsenal Mathieu Debuchy

Beki wa Arsenal Mathieu Debuchy,ameachwa nje ya uwanja kwa wiki sita kutokana na jereha la nyuma ya goti.

Beki huyo wa kulia kutoka faransa, 31,ameshiriki mechi moja tangu mwezi Novemba 2015 walitoka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Bournemouth, lakini mfaransa huyo alitolewa uwanjani baada ya dakika 16.

''Debuchy, amekasirishwa na jeraha hilo lakini ni mtu wa kujikaza na atarudi uwanjani tena,'' amesema meneja Arsene Wenger.

Tuko mwezi wa Disemba,na hata kuwepo hadi katikati mwa mwezi Januari.Hupona haraka kinyume cha matarajio ya wengi.

Habari hizo zimeebuka siku moja baada ya klabu hiyo kudhibitisha kuwa kiungo wa kati Santi Cazorla anatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa fundo la mguu utakao mfanya kusalia nje kwa muda wa miezi mitatu.

Beki Hector Bellerin,pia yuko nje na jeraha la kifundo cha mguu.