Vikosi vya Syria kusitisha mapigano

Vikosi vya Syria
Image caption Vikosi vya Syria

Urusi imesema kuwa vikosi vya Syria vimesitisha operesheni ya kuwasaka waasi mashariki mwa mji wa Aleppo ili kuwezesha raia kuondoka katika eneo hilo la mapigano.

Hata hivyo taarifa kutoka maeneo ya jirani na Aleppo zinasema kuwa japokuwa kuna taarifa kuwa mapigano yamesitishwa hakuna dalili kuwa hali imetulia kabisa.

Mjini New York, ujumbe wa umoja wa mataifa umesema kuwa kusitishwa kwa mapigano hayo kutaleta fursa ya mazungumzo ya amani.

Lakini Staffan de Mistura amesisitiza kuwa mbali na mapigano suala la amani linatakiwa kujadiliwa kivyake.

Wataalamu katika vikosi vya Urusi Pamoja na Marekani wanatarajia kukutana siku ya jumamosi kujadili suala hilo.