Michael Jordan ashinda kesi dhidi ya kampuni ya kichina

Michael Jordan
Image caption Michael Jordan

Mahakama kuu ya China imempa ushindi Mchezaji wa mpira wa Kikapu Michael Jordan katika Kesi ambayo Jordan alikuwa anaishitaki kampuni ya Kichina inayotumia jina lake kujiingizia kipato.

Michael Jordan tangu mwaka 2012 alianza malalamiko dhidi ya Kampuni ya Qiaodan Sports.

Ampapo kampuni hiyo ilikuwa ikitumia jina lake kuuza bidhaa zenye jina la Jordan lakini kwa kichina "Chee-ow-dahn." Mchezaji huyu amesema amefurahi kuona jina lake linaheshimiwa.

Ingawa Mahakama imewaambia wachina wasitumie hilo jina la Jordan kwa kichina lakini wamewaachia mwanya kuwa wanaweza kuandika jina hilo kwa herufi za kirumi Qiaodan"Chee-ow-dahn."