Uchina kuboresha uchunguzi wa anga za mbali kwa ajili ya ulinzi wake

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Uchina ilifanya majaribio yake ya pili ya maabara ya safari za anga za mbali na inapanga kuwa na kituo cha kudumu cha anga kwenye uzio wa sayari ifikapo mwaka 2020.

Serikali ya Uchina imeainisha mipango yake ya maendeleo kwa ajili ya sekta yake ya anga za mbali na kulijenga taifa hilo katika sekta za anga.

Kulinga na sera yake kuhusiana na mikakati hiyo mpango wa haraka wa maendeleo ya safari za anga za mbali autawezesha taifa hilo kuwa na uhakika wa usalama wa taifa pamoja na maendeleo ya kiuchumi.

Sera hiyo imerejelea juhudi za serikali za matumizi ya uchunguzi wa amani wa anga za mbali, licha ya kwamba Marekani inasema Uchina inaweza kutumia uwezo wake kuzuwia mahasimu wake kutumia zana za anga wakati wa mzozo.

Uchina ilifanya majaribio yake ya pili ya maabara ya safari za anga za mbali na inapanga kuwa na kituo cha kudumu cha anga kwenye uzio wa sayari ifikapo mwaka 2020.

Miongoni mwa mipango yake ya baadae ni pamoja na kutua kwa mara ya kwanza kwa chombo chake katika sehemu nyeusi ya mwezi na kutuma chombo chake kwenye sayari ya Mars.