Wafungwa wa Guantanamo Bay wawasili Saudi Arabia

Wafungwa hao walikuwa wakitokea katika mataifa mbalimbali
Image caption Wafungwa hao walikuwa wakitokea katika mataifa mbalimbali

Kundi la wafungwa wa Yemen waliozuiliwa nchini Marekani katika Gereza la Guantanamo Bay wamewasili nchini Saudi Arabia.

Waandishi kutoka katika shirika la habari la AFP wamesema watu watatu wameonekana wakipokelewa na familia zao katika uwanja wa ndege ambao kwa kawaida hupokea viongozi Mashuhuri katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Riyadh.

Kuhamishwa kwa wafungwa kumetokea siku mbili baada ya Ikulu ya Marekani kuahidi kuendelea na mpango wake wa kuhamisha wafungwa kutoka kataka Gereza la Guantanamo Bay, wakipinga suala ambalo limekuwa likipingwa vikali na Rais mteule wa Marekani Donald Trump.