Wanajeshi walioasi Ivory Coast warudi kambini

Waziri wa Ulinzi, Alain Richard Donwahi (aliyeketi kati kati) alizuiliwa kwa saa kadhaa na wanajeshi walioasi Haki miliki ya picha AFP
Image caption Waziri wa Ulinzi, Alain Richard Donwahi (aliyeketi kati kati) alizuiliwa kwa saa kadhaa na wanajeshi walioasi

Wanajeshi wa Ivory Coast wamerudi makambini, na hivo kumaliza uasi wa siku mbili, za uasi ulitapakaa hadi sehemu nyengine za nchi.

Hatua hiyo inafuatia tangazo la Rais Alassane Ouattara, kwamba amefikia makubaliano kuhusu pato lao na marupu-rupu.

Piya pia aliwaomba wanajeshi warudi makambini.

Uasi huo ulitapakaa hadi sehemu nyengine za nchi, lakini wakaazi wa miji iliyoathirika , wanasema maisha yamerudi katika hali ya kawaida, na kwamba barabara na maduka yamefunguliwa.

Waziri wa Ulinzi, Alain Richard Donwahi, ameachiliwa huru, baada ya kuzuiliwa kwa saa kadha, na wanajeshi ambao walikuwa hawakuridhika na mapendekezo ya serikali.

Image caption Ivory Coast