Gambia: Yahya Jammeh amteua mpatanishi

Yahya Jammeh ameteua mpatanishi kusaidia kutatua mzozo wa kisiasa uliopo nchini Gambia Haki miliki ya picha AFP/getty
Image caption Yahya Jammeh ameteua mpatanishi kusaidia kutatua mzozo wa kisiasa uliopo nchini Gambia

Katika kile kinachoonekana kama ishara kuwa Rais wa Gambia ana nia ya kuondoka madarakani, Yahya Jammeh amemteua mpatanishi kusaidia kutatua mzozo wa kisiasa uliopo nchini humo.

Kwenye hotuba kwa taifa Jammeh amesema kuwa ameamrisha buge a wizara ya sheria kubunia sheria ambayo itazuia watu kuandamwa, amabapo pia aliwataka watu kusameheana hasa katika nyanja za kisiasa.

Hata hivyo Jammeh amesisitiza kuwa nchi yake ni lazima isubiri mahakama ya juu kutoa uamuzi kuhusu nani alishinda uchaguzi wa mwezi uliopita.

Hii inafuatia tangazo la siku ya Jumanne kuwa mahakama haitaweza kusikiliza kesi hiyo hadi mwezi Mei wakati jaji raia wa Nigeria aliyeteuliwa kuongoza jopo la majaji atakuwa na muda.

Akitoa hotuba kupitia kwa televisheni ya Gambia, bwana Jammeh alipinga uingiliaji kutoka kwa mataifa ya kigenia baada ya uchuguzi ulioshindwa na mgombea wa upinzani Adama Barrow.

Ametaka kila mmoja kuheshimu sheria na kuisubiri mahakama kuu kutoa uamuzi wake kuhusu uchaguzi huo.

Amelaumu umoja wa mataifa na Ecowas kwa kuchukua maamuzi makali kufuatia uchaguzi huo.