Tiba ya jeni yatoa matumaini kwa viziwi

Haki miliki ya picha Thinkstock
Image caption Viziwi kuanza kusikia hata minong`ono

Panya mwenye matatizo ya kusikia, amefaulu kusikia mnong`ono wa sauti ya chini mno, baada ya kupewa tiba ya "kihistoria" na wanasayansi nchini Marekani.

Wanasema kuwa kurejesha tena uwezo karibu wa kusikia kwa wanyama, kumeleta matumaini kwa matibabu sawa na hayo kwa binadamu "hivi karibuni".

Utafiti huo uliochapishwa katika jarida la asili la Biotechnology, unaelezea marekebisho ya makosa yanayochangia vijinywele vya ndani ya masikio ambavyo vinatumika kunasa sauti kushindwa kufanya kazi.

Watafiti hao walitumia kirusi cha kujiundia kuingizwa ndani ya sikio na kurekebisha matatizo hayo.

"Ni jambo jipya ambalo halikujulikana zamani, ni mara ya kwanza kushuhudia kiwango hiki cha kurejesha uwezo wa kusikia," amesema mtafiti Dkt Jeffrey Holt, kutoka Hospitali ya watoto ya Boston.

Uharibifu wa vijinywele.

Haki miliki ya picha BOSTON CHILDREN'S HOSPITAL
Image caption Kushoto: Sikio nzuri lenye vijinwele sawa. Katikati: Vijinwele vya masikioni vyenye matatizo. Kulia: Vijinywele vya ndani ya masikio vilivyorekebishwa

Nusu ya matatizo ya masikio yasio na uwezo wa kusikia, hutokana na makosa katika maumbile maishani, hasa kwenye chembe chembe za DNA.

Katika majaribio kwenye utafiti huo kwenye Hospitali hiyo ya watoto ya Boston na Chuo cha mafunzo ya matibabu cha Harvard, panya alikuwa na matatizo katika gini maarufu kwa jina Usher syndrome.