Djibril Cisse, astaafu na kuwa DJ

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Cisse aliifungia Liverpool mabao 13 kati ya mwaka 2004 and 2007

Mshambulizi wa zamani wa Liverpool na Ufaransa Djibril Cisse, amestaafu kutoka kwa soka akiwa na umri wa miaka 35.

Awali Cisse alisitisha taaluma yake ya kusakata dimba mwezi Oktoba 2015 kutokana na jeraha la nyonga, lakini alitazamia kurejea baada ya upasuaji.

Aliendelea kufanya mazoezi na klabu yake ya Auxerre katika harakati ya kujiimarisha, lakini baada ya kushindwa kusajiliwa, aliamua kufikisha tamati taaluma yake ya miaka 17.

Cisse, sasa anaangizia taaluma nyingine mpya "kama produza wa Muziki, DJ, na mchambuzi wa Soka.

"Nimependa mno kuwa mwanasoka," anasema. "hadi kufikia sasa, mpira umekuwa ndio maisha yangu.

"Ningependa saana kuendelea na taaluma yangu, lakini inafaa nikiri hapa leo kuwa kandanda imemalizika."

Cisse, aliyeshinda makombe 41 katika rubaa za kimataifa, akiichezea Liverpool kwa miaka mitatu tangu mwaka 2004, kabla ya kurejea katika timu yake ya nyumbani huko Ufaransa - Marseille.

Pia aliwahi kusakatia soka timu za Sunderland, Panathinaikos, Lazio, QPR, Kuban Krasnodar na Bastia.