IAAF, yapiga marufuku wanariadha kubadili uraia

Abraham Rotich wa Bahrain akikabiliana na wakenya David Lekuta Rudisha katika mbio za mita 800 kwenye mashindano ya Dunia mjini Beijing, 2015 Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Abraham Rotich wa Bahrain akikabiliana na wakenya David Lekuta Rudisha katika mbio za mita 800 kwenye mashindano ya Dunia mjini Beijing, 2015

Wanariadha sasa wamepigwa marufuku kubadili uraia kutoka nchi moja hadi nyingine, hayo ni kutokana na mapendekezo yaliyotolewa na Rais wa shirikisho la riadha dunani (IAAF), Lord Sebastian Coe, ambaye amesema kuwa wanariadha ndio "wahusika wakuu" katika tabia hiyo.

"Imekuwa wazi kuwa, uhamisho wa mara kwa mara wa wanariadha, hasa kutoka bara la Afrika, kuwa sheria hii mpya sharti ifuatwe bila majadiliano yoyote," amesema.

Image caption Paul Chelimo anakimbilia Marekani

Wanariadha wa Kenya na Ethiopia wanatazamiwa kuathirika pakubwa kutokana na marufuku hiyo ya kubadilisha uraia kiholela.

Chama cha riadha - IAAF kinasema kuwa, mabadiliko katika sheria ya sasa, yana nia ya kutoa ulinzi wa kutosha kwa wanariadha.

Marufuku hiyo inaanza kutekelezwa mara moja na itaendelea hadi mwisho wa mwaka huu, lakini haitatatiz maombi ya uraia ambayo tayari yanywa na yanaendelea kushughulikiwa.

Mwaakilishi wa bara Afrika katika baraza la IAAF, Hamad Malboub, anasema: "hatua hii ya sasa mbaya. Tulio nayo ni soko kuu la Jumla kwa vipawa vya waafrika kuwekwa wazi kwa mnunuzi wa kiasi kikubwa cha pesa.

"Maslahi ya wanariadha wengi binafsi, wengi wao wanabadili uraia wakingali bado wachanga, hawana habari kabisa kwamba wanakimbia nchi zao."

Zaidi ya wanariadha 20 waliozaliwa nchini Kenya, waliwakilisha mataifa mengine katika mashindano ya olimpiki ya huko Rio mwaka jana.