Michezo miwili ya Vpl kupigwa leo

TFF Haki miliki ya picha Google
Image caption Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania

Michezo miwili ya ligi kuu Tanzania bara itapigwa leo katika mkoa ya mtwara na Jiji la Mbeya.

Ndanda Fc ya Mtwara watakua nyumbani katika dimba Nangwanda Sijaona kuwakaribisha Mbao Fc kutoka mkoani Mwanza.

Tanzania Prisons ya Jijini Mbeya watakua wenyeji wa Kagera Sugar ya Mkoani Kagera mchezo huo utapigwa katika dimba la Sokoine

Mechi nyingine za ligi hiyo zitaendelea Februari 17, 18 na 19 kwa mujibu wa Ratiba.