Wakenya wawika mbio za Berlin Marathon

Eliud Kipchoge
Image caption Eliud Kipchoge

Mwanariadha wa Kenya, Eliud Kipchoge, amethibitisha kuwa yeye ni kidedea wa dunia katika mbio ndefu, kwa kuibuka mshindi wa mbio za Berlin Marathon.

Alimaliza mbio hizo kwa saa mbili na dakika 34, na kumpiku mpinzani wake wa karibu Guye Adole wa Ethiopia.

Rekodi ya dunia ya mbio hizo, imekuwa ikivunjwa mara saba huko huko Berlin, katikia kipindi cha miaka 20 iliyopita kutokana na hewa nzuri kwa mbio hizo na babara kuwa tambarare.

Mwezi Mei Kipchoge alibakisha sekunde 25 tu kukimbia muda wa chini ya saa mbili mbio za marathon katika warsha iliyoandaliwa huko Monza nchini Italia.

Upande wa wanawake Mkenya Gladys Cherono aliibuka mshindi alipotimka mbio hizo kwa muda wa saa 2:20:23 naye Muithiopa Ruti Aga akamaliza wa pili kwa 2:20:41.

Mada zinazohusiana