Ushindi usio rahisi wa Mancity dhidi ya Donetsk

De Bruyne aifungia Mancity bao lake la kwanza la msimu Haki miliki ya picha Reuters
Image caption De Bruyne aifungia Mancity bao lake la kwanza la msimu

Mabingwa wa Ukrain Shakhtar walidhihirisha kuwa timu bora kuwahi kupambana na City msimu huu na mabingwa hao walikabiliwana kibarua kigumu kabla ya ya kufanikiwa kukusanya pointi tatu.

City walitarajiwa kuwanyorosha wapinzani wao lakini walighdhabishwa kwa ufunguzi wa kipindi cha kwanza bila ya kufunga bao.

Kevin de Bruyne alifunga goli lake safi la kwanza la msimu baada ya kubadilishana pasi na David Silva.

Raheem Sterling aliongeza la pili la dakika za mwisho na kufanikisha ushindi huo dhidi ya Shakhtar Donetsk na ushindi wa mara ya pili katika ligi ya mabingwa kwenye kundi F kati ya mechi mbili.

Shakhtar wenyewe walikuwa na fursa, kombora la mchezaji wa Brazil Marlos lililokolewa na kipa Ederson huku mshambuliaji wa zamani wa Newcastle Facundo Ferreyra akipiga hedi ilioponyoka kutoka yadi sita nje.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii