Mshambuliaji wa ManCity Sergio Aguero ajeruhiwa katika ajali

AJALI YA AGUERO Haki miliki ya picha KAWILIKO MEDIA

Mshambuliaji wa Manchester City Sergio Aguero amejeruhiwa katika ajali ya barabarani mjini Amsterdam, saa chache baada ya kuhudhuria tamasha.

Raia huyo wa Argentina, mwenye umri wa miaka 29, anaarifiwa kuwa ndani ya taxi akielekea katika uwanja wa ndege baada ya kuhudhuria tamasha la muimbaji Maluma.

City imesema "alikuwa Uholanzi katika siku yake ya mapumziko na amepata majeraha".

Image caption Sergio Aguero

Aguero anatarajiwa kurudi Manchester Ijumaa na atakaguliwa na kikosi cha madaktari wa City kabla ya kuelekea kwa mchuano wa Premier League watakapokaribishwa na Chelsea Jumamosi.

Polisi Amsterdam wameithibitishia BBC kwamba watu wawili walikuwa ndaniya taxi iliyohusika katika ajali katika eneo la De Boelelaan mjini humo.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii