Mali na Ghana zatinga kumi na sita bora

Heka heka za vijana katika mchezo dhidi ya New Zealand Haki miliki ya picha Google
Image caption Heka heka za vijana wa Mali katika mchezo dhidi ya New Zealand

Wawakilishi wa Afrika katika michuano ya kombe la dunia la vijana la chini ya miaka 17 timu za Mali na Ghana zimetinga hatua ya kumi na sita bora ya michuano hiyo.

Mali walioko katika kundi B wamemaliza katika nafasi ya pili nyuma ya Paraguay kwa baada ya kuichapa Zew Zealand kwa mabao 3-1.

Ghana wakawaondosha wenyeji India, kwa kuwachapa kwa mabao 4-0, na hivyo Ghana kuongoza kundi A kwa Alama sita wakifuatiwa na Colombia.

Paraguay wakawachapa Uturuki kwa mabao 3-1 na Colombia wakaibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Marekani.