Mafunzo kutoka safari yangu ya Antaktiki

Erasto Enyawike Haki miliki ya picha Erasto Enyawike
Image caption Erasto Enyawike, Mtanzania aliyetembelea bara la Antaktiki

Erasto Enyawike ni mwanaharakati wa mazingira kwa zaidi ya miaka 30 kutoka Tanzania.

Alipata fursa ya kutembelea bara la Antaktiki mara baada ya kushinda safari hiyo kupitia mradi wa roots and shoots kutoka taasisi ya Dr Jane Goodall.

Antaktiki ni bara lililopo kwenye ncha ya kusini ya dunia, kati ya bahari za Pasifiki, Atlantiki na Bahari Hindi.

Bara hili linajulikana kama jangwa baridi.

Kwa sababu ya baridi kali katika bara hilo, ni bara pekee ambako binadamu hawaishi kwa namna ya kudumu, isipokuwa kuna watu 5,000, hasa wanasayansi, wanaokaa kwa muda katika vituo vyao.

Akizungumza na mwandishi wa BBC Munira Hussein, na kuelezea mambo matatu aliyojifunza kutoka safari yake.

Haki miliki ya picha Erasto Enyawike
Image caption Bara Antaktiki linajulikana kama jangwa baridi.

1. 'Maaumuzi magumu'

Kwenda Antaktiki ni moja kati ya maamuzi magumu na ya kijinga ni kutembelea bara hili lakini, sijutii lakini ni safari yenye faraja kubwa na nimejifunza mengi sana.

Nimeona mabadiliko ya tabia nchi barani humo, ambapo kulikua na barafu zenye urefu lakini ongezeko la joto limesababisha barafu hizo zimeyayuka.

Haki miliki ya picha Erasto Enyawike
Image caption Wanaharakati mbalimbali wa mazingira wamekua wakifanya jitihada mbalimbali za kupambana na mabadiliko tabia ya nchi.

2. 'Wakimbizi wa mazingira'

Mabadiliko ya bara hilo yanaweza kuathiri dunia nzima, na ikiwa maji ya bara la artantiki yatayeyuka basi huenda Tanzania inaweza kuzama au Kenya, lakini pia tutaanza kupokea wakimbizi wa mazingira mbali na tuliyozoea kuwa na wakimbizi wa migogoro na vita.

Mtazamo wangu umebadilika sana mara baada ya safari hii, tumekua tukiangalia dunia kama kitu kingine na si sehemu ya maisha, lakini baada ya safari hii sasa naona dunia ni kama sehemu ya maisha na tusipokua makini basi tunaingia katika hatari kubwa.

Haki miliki ya picha Erasto Enyawike

3. 'Mwisho wa dunia'

Katika safari hii, sehemu ya kwanza ilinishtua ni sehemu tulifika tukakuta kibao kimeandikwa 'end of the world' yaani mwisho wa dunia. Na tulipita katika mkondo hatari wenye bahari chafu sana, hivyo masaa 48 ya kwanza ilikua ni kuomba Mungu.

Bara hili lina eneo la kilomita za mraba milioni 14 na eneo hili limefunikwa karibu kabisa, yaani kwa asilimia 98 ya eneo na theluji na barafu. Eneo lake ni kubwa kushinda Ulaya lakini hakuna mti hata mmoja.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii