Namna Brexit utakavyoathiri soko la Kenya
Huwezi kusikiliza tena

Namna Brexit utakavyoathiri soko la Kenya

Viongozi wa Jumuiya ya madola wamekuwa na mkutano kwa wiki nzima kujadili maswala mbali mbali ikiwemo biashara. Kwa muda wa chini ya miaka miwili, Uingereza imekuwa katika vuguvugu la kutaka kujitoa katika umoja wa Ulaya jambo ambalo bila shaka litayaathiri mataifa yaliyo katika jumuiya ya madola.

Anne Soy, amezuru mashamba nchini Kenya yanayouza maua,mboga na matunda katika nchi za Ulaya ili kujua mpango wa Brexit utawaathiri vipi.