Alex Ferguson afanyiwa upasuaji wa dharura

Uingereza,sir Alex Furgerson Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Meneja wa zamani wa timu Manchester United Alex Ferguson

Meneja wa zamani wa timu Manchester United Alex Ferguson alifanyiwa upasuaji wa dharura mwishoni mwa wiki iliyopita kutokana na tatizo kwenye ubongo wake unaotishia kumletea kiharusi.

Ugonjwa huo unatokana na mtu kupata tatizo la damu kuvuja ndani ya ubongo wake na ni moja ya ugonjwa hatari sana unaoweza kusababisha kifo.

Taarifa kuwa upasuaji huo umefana kwa kiasi kikubwa, ingawa Ferguson anahitaji muda wa unagalizi wa hali ya juu ili kuboresha ahueni yake .

Furgerson mwenye miaka 76 , alistaafu akiwa meneja wa Manchester United mnamo mwezi May mwaka 2013 baada ya kuiwezesha timu hiyo kutwaa makombe 38 katika kipindi cha miaka 26 cha uongozi wake.

Kwa mara ya mwisho alionekana kwenye uwanja wa Old Trafford alipokuwa akimpa tuzo ya heshima nakukumbukwa bosi wa timu ya Arsenal , Arsene Wenger

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Alex Ferguson na Arsene Wenger walipokuwa pamoja katika viwanja vya Old Trafford mwishoni mwa wiki

Familia ya Furguson imeomba kupewa muda wa kumhudumia mgonjwa zaidi wakati anapopata ahueni katika hospitali ya Salford Royal.

Tutawaombea mgonjwa Alex na wapendwa wake katika kipindi hiki na tunaungana pamoja katika kuomba na kuona akipona kwa haraka

Ferguson anaelezwa kama meneja aliyefanikiwa zaidi katika historia ya mchezo wa soka nchini Uingereza, Mashindano ya Ferguson huko Old Trafford ni pamoja na majina 13 ya Ligi Kuu ya Kwanza.

Salamu za pole na nyingi za kumuombea uponyaji wa haraka zimekuwa zikimiminika kila kona nchini humo kutoka kwa wachezaji nguli wa soka likiwemo shisirikisho la soka ulimwenguni nalo limetoa salamu kumtakia uponaji wa haraka.

Ferguson alimuoa mkewe Cathy tangu mwaka 1966, mwanawe wa kiume Darren ni meneja wa timu ya Doncaster Rovers ambayo ilishindwa kufufua dafu kileleni mwa ligi yao dhidi ya timu ya Wigani mwishoni mwa wiki .