Saud Arabia kurekebisha sheria zake

Saudi Arabia
Image caption Mtawala Mkuu Mohammed bin Salman wa Saudi Arabia

Wanaharakati wa haki za binaadamu , Human Rights Watch, wenye asili ya Marekani, wameishutumu Saud Arabia kwa kuwaweka kizuizini maelfu ya watu kwa muda wa miaka kumi bila kufikishwa mahakamani.

Kikundi hicho kinasema data rasmi kutoka kwa wizara ya mambo ya ndani ya nchi hiyo inaonyesha kuwa zaidi ya watu elfu mbili na miatatu walifungwa kwa zaidi ya miezi sita bila hukumu na wengine wameshikiliwa hadi miaka kumi.

Mkuu wa nchi hiyo, Mtawala Mkuu Mohammed bin Salman, ameanzisha mageuzi makubwa katika miezi iliyopita katika jaribio la kufanyia marekebisho sheria zake ili kuendana na hali ilivyo ulimwengunidhidiya ufalme wa kihafidhina.

Human Rights Watch inasema kuwa, licha ya hali hiyo , idadi ya watu waliofungwa kwa muda mrefu sana inaonekana inaongezeka kwa kiasi kikubwa katika miaka ya hivi karibuni.