Polisi wavunja maandamano Zimbabwe

Waandamanaji wamtaka Mugabe ajiuzulu Haki miliki ya picha AFP
Image caption Polisi watumia nguvu kuvunja maandmano Zimbabwe

Maafisa wa polisi wa kupambana na ghasia nchini Zimbabwe wametumia gesi ya kutoa machozi na maji, kutawanya mamia ya waandamanaji katika mji mkuu Harare.

Waandamanaji hao, waliokuwa na nia ya kuelekea hadi kwenye makao ya bunge kutoka upande wao walirusha mawe

Haki miliki ya picha AP
Image caption Waandamanaji walibeba mabamngo ya kumtaka Mugabe ajiuzulu

Waliandamana huku wakipeperusha mabango yenye maandishi "Rais Mugabe lazima ang'atuke" na "umefeli bwana Mugabe"

Wanafunzi wa vyuo vikuu walikuwa miongoni mwa waandamanaji, na wanasema maandamano hayo hayakuchochea vurugu.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Polisi watumia nguvu kuvunja maandamano

Baadhi ya waandamanaji wanapinga mpango wa serikali kuanzisha noti nyenginezo aina ya zile zinazoitwa 'bond notes' ambayo inasemekana italingana na thamani ya dolla ya Marekani.

Uchumi wa Zimbabwe umekumbwa na mdororo wa mda mrefu kiasi cha sarafu ya nchi hiyo kukosa thamani pakubwa.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Polisi walitumia nguvu kuwatawanya waandamanaji

Mwezi jana chama cha ma- veteran wa vita vya ukombozi wa Zimbabwe ambacho kimekuwa kikimuunga mkono kwa dhati rais Mugabe, kilikumbwa na mgawanyiko huku wengine wakikashifu vikali sera za Mugabe wakisema ndizo zilizosababisha uchumi wa nchi hiyo kuanguka vibaya sana.