Kwa Picha: Kufanya mazoezi

Wengi wetu tunafahamu kwamba kufanya mazoezi huusaidia mwili kuwa katika hali nzuri. Hata hivyo, bado huwa vigumu kwetu kufanya mazoezi.Mpiga picha Ed Gold aliamua kuchunguza ni nini huwapa msukumo watu kutembelea chumba cha mazoezi cha Anytime Fitness, eneo la Colchester nchini Uingereza na akawahoji baadhi ya watu.

Grey line

Jo Nicholls

Jo Nicholls Haki miliki ya picha Ed Gold

Nina watoto wawili, hivyo mimi huja hapa ili mwili wangu uwe katika hali nzuri na niweze kula nitakacho bila wasiwasi.

Napenda pizza na vyakula vingine vitamu tamu.

Huwa naishi vyema siku za wiki, kufanya mazoezi na kula chakula chenye afya lakini wikendi niko huru kula chochote nitakacho.

Mazoezi hukufanya ujihisi vyema zaidi, na kujiamini hata zaidi.

Grey line

Daniel McTaggart

Daniel McTaggart Haki miliki ya picha Ed Gold

Nilitaka mwili wangu uwe mzuri, na miaka miwili iliyopita, baada ya kuhusika katika ajali ya barabarani niliumia shingo. Ilinibidi kwenda mazoezini kuongeza nguvu shingoni.

Lakini sasa naenda kwa raha zangu. Sitaki kuwa mtu ambaye hawezi kuinua kapu baada ya kununua vitu dukani. Sana, nafanya mazoezi ili mwili wangu uwe katika hali nzuri na pia kwa ajili ya familia yangu na mimi binafsi.

Grey line

Lauren Abrey

Lauren Abrey Haki miliki ya picha Ed Gold

Mwanzoni, nilifika chumba cha mazoezi ili kupunguza uzani, lakini sasa naja kwa sababu ni jambo ninalolipenda na kulifurahia.

Nikianza na mazoezi basi ninaweza kuendelea na siku yangu vyema, kutazama mabadiliko yakitokea kwenye mwili wangu. Hili hunifanya nitake kurudi siku baada ya siku. Hili linahitaji kujitolea.

Mimi hufurahia kuja hapa kwa mazoezi. Mpenzi wangu hupenda kwenda kucheza gofu, mimi naye hupenda kuja hapa.

Grey line

Tetteh Apedo

Tetteh Apedo Haki miliki ya picha Ed Gold

Huwa nafanyanya mazoezi kuweka mwili wangu katika hali nzuri na kuwa na afya njema.

Nilizoea kukimbia sana nikiwa Ghana, na mazoezi ya mwili asubuhi.

Huwa ninafuraha sana ninapotembelea chumba cha mazoezi.

Kuwa na mwili mzuri hukufanya pia unajaimini zaidi. Ninataka kuwa mfano mwema kwa watoto wangu.

Grey line

Luis 'Lu' Hurley

Luis Hurley Haki miliki ya picha Ed Gold

Nimekuwa nikifanya mazoezi kwa miaka miwili unusu, mara kwa mara nikipumua. Muhimu kwangu ni kuwa na mwili mzuri na kuujaribu mwili wangu kiakili.

Ni vizuri kuuweka mwili wako kwenye shinikizo na kuona unaweza kuhimili hadi wapi.

Ukizoea kufanya, inakuwa kama uraibu.

Ukimwuliza mtu yeyote chumba cha mazoezi, atakwambia kwamba anafurahishwa na mwonekano wa mwili wake.

Grey line

Emily Meadows

Emily Meadows Haki miliki ya picha Ed Gold

Nadhani ni jambo zuri sana la kupunguza msongo wa mawazo. Ndio tu nimemaliza masomo chuoni. Na sasa mitihani imekwisha, huwa naja hapa ndipo nipate kitu cha kufanya.

Nilijiunga na kituo hiki pamoja na marafiki zangu, lakini wote walijiondoa kwa sababu hawakuwa na hamu.

Grey line

Kristie Theobald

Kristie Theobald Haki miliki ya picha Ed Gold

Mimi ni mwanafunzi wa chuo kikuu hapa, nasomea lugha ya Kiingereza. Baadaye nitasomea ualimu na natumai kwamba mwishowe nitakuwa mwalimu wa shule ya upili.

Mpenzi wangu ndiye aliyenihamasisha.

Tayari nimekuwa mwembamba, kwa hivyo huwa nafanya mazoezi mengine badala ya cardio. Lakini sifanyi mazoezi ndipo nijenge misuli.

Kuweza tu kuinua mizigo mizito ni jambo ambalo kwangu ni ufanisi mkubwa.

Grey line

James Ferguson

James Ferguson Haki miliki ya picha Ed Gold

Nilitaka kufanya mazoezi kwa manufaa yangu binafsi na si kwa sababu ya kujionesha na kujipendekeza kwa watu.

Lakini furaha ya kuwa na watu mia kadha mbele yako na pia kuonesha matokeo ya mazoezi uliyoyafanya vilinifanya kuzoea.

Huwa sinyanyui uzani mzito. Ni kwa kipimo tu na kula vyema.

Grey line

Nick 'Murphy' Maxwell

Nick Maxwell Haki miliki ya picha Ed Gold

Nimekuwa nikifnaya mazoezi kwa zaidi ya miaka 20 tangu nianze kutumia chumba cha kufanyia mazoezi. Mke wangu ni mwalimu wa mazoezi.

Nilicheza kidogo na uzani miaka yangu ya 20 lakini sasa natia bidii sana na vipimo vya uzani hapa ni bora.

Kufanya mazoezi kuna manufaa mengi, hasa utakapozeeka. Hukufanya bado uwe na nguvu, mgongoni, moyo na pia mapafu. Na labda huzuia ugonjwa wa kupoteza fahamu uzeeni.

Grey line

Megan Slade

Megan Slade Haki miliki ya picha Ed Gold

Niko hapa kupunguza uzani baada ya kujifungua mtoto ndipo nguo nilizozoea kuzifaa awali ziweze kunitosha. Pia husaidia kiakili, kupoteza fikira baada ya kusumbuka na mtoto.

Na pia hupunguza hatari ya maradhi ya moyo.

Nilikutana na mchumba wangu chumba cha mazoezi. Huwa unajua mtu atakupenda iwapo ataendelea kupendezwa nawe hata baada ya kukuona ukiwa katika hali ambayo si nzuri, umejaa jasho na hujajipodoa.

Grey line

Ashley Perkins

Ashley Perkins Haki miliki ya picha Ed Gold

Niligundua kwamba nilikuwa naugua ugonjwa wa Kisukari Aina-1 mwezi mmoja kabla ya kutimiza miaka 21. Huwa najidunga homoni mara sita kwa siku.

Unapofanya mazoezi, mwili wako hutoa endorphins, ambazo husaidia kupunguza mfadhaiko wa kiakili.

Nilizoea kuwa na msongo wa mawazo na kukasirika haraka lakini siku hizi nimebadilika.

Grey line

Kelly Doherty

Kelly Doherty Haki miliki ya picha Ed Gold

Huwa inakuwa kama uraibu. Ni muhimu kwangu sasa kwa sababu sipatwi na msongo wa mawazo tena. Huwa naudhika sana ninapokosa mazoezi hata siku moja.

Bora tu usipoteze msukumo, utaendelea kurudi tena na tena.

Sitaki hii dhana kwamba wanawake hutazamwa kama watu wadhaifu. Nataka niwe mtu anayeweza kuinua mizigo mizito.

Grey line

Emma Paveley

Emma Paveley Haki miliki ya picha Ed Gold

Nilikuwa mtu mfanya mazoezi kama mchezo tangu nikiwa na miaka tisa hadi nilipotimu miaka 16. Nilifanya vyema sana. Nilizoea kufanya mazoezi saa 20 kwa wiki.

Huwa napenda sana, ninaweza kusema ni jambo limo ndani ya mwili wangu.

Nilishinda tuzo ya ubingwa wa KBFF [UK Body Building and Fitness Federation] mara mbili.

Huwa nashiriki shindano, napata ushauri na kuendelea na kujiimarisha zaidi.

Grey line

Picha zote na © Ed Gold

Mada zinazohusiana