Afrika Kusini: ANC yakabiliwa na ushindani mkali

Raia wa Afrika Kusini wapiga kura
Image caption Raia wa Afrika Kusini wapiga kura

Huku nusu ya kura zikiwa zimehesabiwa kwenye uchaguzi wa Afrika Kusini chama tawala cha African National Congress ANC kinakabaliwa na ushindani mkali zaidi tangu kiondoe utawala wa ubaguzi wa rangi mwaka 1994.

Tayari kimepata asilima 50 ya kura hizo hadi sasa huku mpinzani wake mkubwa chama cha Democtratic Alliance kikijipatia asilimia 34.

Katika uchaguzi wa Mabaraza miaka mitano iliyopita ANC ilishinda thuluthi mbili ya kura.

Ukosefu mkubwa wa ajira na sakata za ufisadi zinazomuandama rais Jacob Zuma na wengine umeathiri umaarufu wa chama hicho.

Mada zinazohusiana