Koffi Olomide atumbuiza Brazzaville

Koffi Olomide Haki miliki ya picha AFP
Image caption Koffi Olomide atumbuiza Brazzaville

Mwanamuziki nyota wa Rhumba kutoka DRC Koffi Olomide aliwatumbuiza mashabiki Brazzaville tamasha la kwanza tangu 'sakata la teke' nchini Kenya kumsababishia kufungwa jela.

Olomide alisambaza video ya sehemu ya shoo yake mjini Brazzaville, katika Jamhuri ya Congo akiwa sako kwa bako na mwanafunzi wake Fally Ipupa.

Olomide alisafirishwa kwenda mjini Kinshasa DRC kutoka Nairobi baada ya kukabiliwa na shutuma baada ya kanda ya video kuenea mitandaoni ikionekana kumuonyesha akimshambulia mwanamke uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta muda mfupi baada ya kuwasili nchini humo.

Mwanamke huyo anadaiwa kuwa mmoja wa wachezaji ngoma wake.

Olomide alikamatwa punde baada ya kuwasili nchini DR Congo.

Hata hivyo alipewa dhamana kufuatia shinikizo la mashabiki wake.