Wahamiaji 21 wazikwa Libya

Wahamiaji 21 waliozama wameripotiwa kuzikwa na wakazi wa mji wa Libya baada ya miili yao kukutwa ikielea ufukweni.

Mamlaka nchini humo zinasema zililazimika kuchukua hatua ya kuondoa maiti zilizokuwa zinazagaa.

Image caption Bahari ya Mediterranea inayotumika na wahamiaji kwenda ng'ambo

Miili hiyo ilikaa siku tatu katika pwani ya Al- Maya, kaskazini mwa Tripoli .

Image caption Mohammed Garbaj amekuwa akijaribu kuwaokoa wahamiaji wanaozama

Wenyeji wa eneo hilo walijawa na hofu ya maiti hizo kusababisha magonjwa ndipo wakalazimika kuzizika.