Wataalamu waonya Trump atakuwa 'rais mropokaji'

Viongozi wa usalama wa kitaifa wa Republican wanasema Bwana Trump "atakua rais asie kuwa makini zaidi katika historia ya Marekanii'' Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Viongozi wa usalama wa kitaifa wa Republican wanasema Bwana Trump "atakua rais asie kuwa makini zaidi katika historia ya Marekanii''

Wataalam hamsini wa masuala ya usalama ambao kwa pamoja wamewahi kuhudumu katika utawala wa Republican wameonya kwamba Donald Trump"atakuwa rais asiekua makini zaidi " kuwahi kuhudumu katika historia ya Marekani.

Katika waraka wao wa wazi wanasema Bwana Trump "hana haiba, maadili wala uzoefu " wa kuongoza nchi.

Kundi hilo la wataalam wa masuala ya usalama linajumuisha mkurugenzi wa zamani wa idara ya ujasusi ya Marekani CIA Michael Hayden na wakuu wa zamani wa usalama wa ndani wa nchi.

Wengi wa waliotia saini waraka huu kuhusu Trump walikataa kusaini waraka kama huo mwezi Machi.

Bw Trump amejibu kwa kusema kuwa waraka huo ni wa wasomi wa Washington waliofeli ambao amesema wanapaswa kulaumiwa kwa kufanya dunia kuwa mahala hatari.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Waliosaini waraka ni pamoja na mkurugenzi wa zamani wa CIA Michael Hayden

Bw Trump amekiuka sera ya kigeni ya Republican mara kadhaa.

Mgombea wa chama cha Republican amehoji ikiwa Marekani inapaswa kuheshimu wajibu wake kwa NATO, kuidhinisha mateso na kupendekeza kwamba Korea Kusini na Japan wanapaswa kujihami kwa silaha za nyuklia .

"Alithoofisha mamlaka ya Marekani inayojitambua kama kiongozi wa dunia huru ," ulieleza waraka wa wakuu hao wa zamani wa usalama.

"Anaonekana kukosa uelewa wa kimsingi kuhusu imani katika katiba ya Marekani, sheria za Marekani na taasisi za Marekani ,ikiwemo uhuru wa kidini, uhuru wa vyombo vya habari, na uhuru wa mahakama. ."

"Hakuna hata mmoja wetu atakaempigia kura Donald Trump," ilielezea barua.

Katika kauli yake Bwana Trump amesema majina ya wale walioandika waraka huo yalikua "ya wale ambao wamarekani wanapasa kuwatafuta kupata majibu ya kwanini dunia imeharibika".

"Tunawashukuru kwa kujitokeza ili kila mmoja nchini atambue ni nani anapaswa kulaumiwa kwa kuifanya dunia kuwa mahala hatari kiasi hiki ," aliendelea.

" Si lolote hao zaidi ya wasomi walioshindwa kazi ambao wanataka kuendelea kushikilia mamlaka na ni wakati sasa wa kuwawajibisha kwa vitendo vyao."

Pia miongoni mwa wale waliotia saini waraka huo ni pamoja na John Negroponte, mkurugenzi wa kwanza wa idara ya ujasusi na baadae naibu waziri wa mambo ya nje; Robert Zoellick, ambae pia alikuwa naibu waziri wa mambo ya kigeni na rais wa zamani wa Benki ya dunia ; na mawaziri wa zamani wa usalama wa ndani ya nchi , Tom Ridge na Michael Chertoff.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii