Watoboa treni na kuiba dola 750 elfu India

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wezi nchini India wametoboa shimo kwenye treni iliyokuwa imebeba pesa na kuiba dola laki saba u nusu.

Wezi nchini India wametoboa shimo kwenye treni iliyokuwa imebeba pesa na kuiba dola laki saba u nusu.

Treni hiyo iliyokuwa ikipitia maeneo ya kusini mwa India ikielekea Chennai safari ya kilomita 300 ilikuwa na polisi waliokuwa wakilinda pesa hizo mali ya benki kuu ya India.

Hata hivyo walinzi hao waliokuwa ndani ya behewa lingine hawakusikia uhalifu huo ukitendeka na sasa wanachunguzwa.

Treni hiyo ilikuwa imebeba dola milioni ($51).

Polisi wanashuku kuwa kati ya wezi 6-8 walishiriki wizi huo kwa kutoboa shimo kwenye paa ya treni hiyo wakitumia kurunzi maalum.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Pesa hizo nzee zilikuwa zimekusanywa iliziharibiwe.

Kurunzi hiyo hutoa miale yenye joto kali linayeyusha hata Chuma bila ya kutoa kelele zozote.

Uchunguzi tayari umeanza.

Inspekta jenerali wa polisi M. Ramasubramani, amenukuliwa akisema ''Tunashuku walitoboa paa ya treni hiyo na wakaiba pesa hizo taslimu jumatatu usiku''

Wizi huo uligundulika Jumanne baada ya treni hiyo kufika mjini Chennai na wahudumu wakagundua kulikuwa na shimo na kisha kiasi cha fedha hizo zilikuwa hazipo.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Polisi waliokuwa wamepewa jukumu la kulinda shehena hiyo hawajui wasema nini

Pesa hizo nzee zilikuwa zimekusanywa iliziharibiwe.

Wizi huo umeibua kumbukumbu ya wizi uliotokea Uingereza mwaka wa 1963 almaarufu "Great Train Robbery" ambapo wezi walisimamisha treni na kuiba pauni milioni 2.6.