Mkuu wa Polisi Uganda akaidi amri ya korti

Image caption Waandamanji wanaounga mkono mkuu wa polisi wa Uganda

Polisi wa kupambana na ghasii nchini Uganda wamewatimua waandamanaji kutoka majengo ya mahakama ambapo mkuu wa polisi nchini humo alikuwa ametakikana kufika kujibu mashtaka yanayohusu kupigwa kwa waandamanaji mwezi uliopita.

Kundi la watu ilikusanyika nje ya mahakama ya Makindye wakiwa na mabango kadhaa yakiwa na maenno kama vile IGP hana kesi huku wakipaza sauti zao nje ya mahakama wakimuunga mkono mkuu wa polisi jenerali Kale Kaihura.

Hata hivyo jenerali Kayihuru na maafisa wengine 7 wa vyeo vya juu hawakufika mahakamani jambo lililomlazimu mwendesha mashataka wa serikali DPP kuomba achukue wadhifa wa kesi hiyo.

Jaji akamuomba atoe ombi rasmi na kuahirisha kesi hiyo hadi Agosti 29 mwaka huu.

Ombi la upande wa walalamishi la kumtaka mkuu wa polisi na wenzake wakamatwe kwa kushindwa kufika mahakamani halikusikizwa ila jaji alisema kuwa atatoa uamuzi wake tarehe 29 Agosti.

Image caption Mkuu wa Polisi Uganda akaidi amri ya korti

Wanalaumiwa kwa kuendesha ukatili dhidi ya wafuasi wa mwanasiasa wa upinzani Kizza Besigye.

Baadhi ya magari ya upande wa ulalamishi yaliharibiwa kwa mawe na wafuasi wa Inspekta huyo mkuu wa polisi.

Takriban mawakili 20 waliwasilisha kesi hiyo kwa niaba ya wale waliopigwa na polisi.

Kesi hiyo ilihairishwa hadi tarehe 29 mwezi huu.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii