Aliyeokolewa kutoka Boko Haram asema anamkosa baba wa mtoto

Rais Buhari alikutana na Amina Ali baada ya kuokolewa Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rais Buhari alikutana na Amina Ali baada ya kuokolewa

Msichana mmoja raia wa Nigeria ambaye aliokolewa kutoka mikononi mwa kundi la wapiganaji wa Kiislamu wa Boko Haram, amesema anamkosa sana mpiganaji wa kundi hilo ambaye ni baba wa mtoto wake.

Amina Ali ni mmoja wa wasichana mia mbili wa shule ya Chibok waliotekwa nyara miaka miwili iliyopita.

Amesema kile anachotaka sasa ni kwenda nyumbani.

Haki miliki ya picha Nigeria Military
Image caption Madaktari wa kijeshi wamchunguza mtoto baada ya kuokolewa

Yeye pamoja na mtoto wake wamekuwa wakizuiliwa katika mjini Abuja, katika kile serikali inasema ni mpango wa kumwezesha kutengamana na watu tena.

Amina Ali alipatikana katika msitu mmoja mapema mwaka huu akiwa na mtoto wake na mtu mmoja ambaye alisema ni mumuwe ambaye ni mpiganaji wa kundi hilo la Boko Haram.