Afisa wa cheo cha juu wa Korea Kaskazini atorokea Korea Kusini

Imethibitishwa kuwa bwana Thae ( kulia) kwa sasa yuko Korea Kaskazini Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Imethibitishwa kuwa bwana Thae ( kulia) kwa sasa yuko Korea Kaskazini

Korea Kusini imethibitisha kuwa afisa mmoja wa kibalozi wa Korea Kaskazini aliyekuwa akihudumu mjini London, ametoroka na sasa yuko mjini Seoul na familia yake.

Thae Yong-ho ambaye alikuwa naibu balozi wa korea kaskazini mjini London, anaaminika kuwa afisa wa serikai ya ngazi ya juu zaidi wa Korea Kaskazini kutangaza rasmi kuwa sio raia wa taifa hilo.

Msemaji wa serikali ya Uchina amesema balozi huyo alitoroka kwa sababu alitaka utawala wa kidemokrasia na wasi wasi kuhusu hatma ya familia yake.

Ubalozi wa Korea Kaskazini mjini London haujatoa tangazo lolote kuhusiana na tukio hilo.