Kikosi cha Watu 10,000 chapambana na moto California

Moto mkubwa wazuka mjini California Marekani Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Moto mkubwa wazuka mjini California Marekani

Zaidi ya wafanyakazi 10,000 wa kikosi cha kuzima moto katika mji wa California wanaendelea kupambana na moto mkubwa katika jimbo hilo.

Maafisa wanasema moto huo mkubwa umesababisha barabara kuu na njia ya reli inayounganisha mji huo na Los Angeles pamoja Las Vegas kufungwa.

Maelfu ya watu wameamuriwa kuondoka katika nyumba zao hata hivyo baadhi wamekataa.

John Miller kutoka kikosi cha huduma za misitu amewataka raia wa nchi kutekeleza amri ya kuondoka.