Mwogeleaji wa Marekani kulipa faini Brazil

Jimmy Feigen alishinda dhahabu katika uogeleaji Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Jimmy Feigen alishinda dhahabu katika uogeleaji

Mwanariadha muogeleaji raia wa Marekani Jimmy Feigen amekubali kulipa karibu dola 11,000 kwa shirika moja la misaada nchini Brazil kufuatia mzozo kuhusu wizi wa kutumia nguvu.

Yeye ni mmoja wa washindi wanne wa medali za dhahabu akiwemo nyota Ryan Lachte ambao taarifa zao ziligonga vyombo vya habari baada ya bwana Lochte kudai kuwa waliporwa wakiwa mjini Rio.

Baadaye picha za CCTV zilibadilisha madai yao zikionyesha kuwa waogeleaji hao walikuwa wameharibu kituo cha mafuta.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Ryan Lachte ni mmoja wa waogeleaji maarufu nchini Marekani

Bwana Lochte aliondoka nchini Brazil siku ya Jumanne lakini Feigen alisalia na kisha kukamatwa.

Wenzao wawili Gunnar Bentz na Jack Conger,walitolea ndania ya ndege mjini Rio siku ya Alhamisi usiku na kuhojiwa ana polisi.

Wanakana kushiriki kwenye madai hayo ya uongo ya wizi na kuruhusiwa kuondoka kwenda Marekani baadaye.

Wakili wa Feigen alisema kuwa makubaliano yameafikiwa na atatoa dola 10,800 kwa taasisi moja na kisha kurejeshewa pasipotia yake ili aweze kusafiri nyumbani.