Taliban wateka wilaya muhimu nchini Afghanistan

Wanamgambo wa Taliban wameteka wilaya muhimu katika mkoa ulio kaskazini mwa Afghanistan wa Kunduz.
Wapiganaji hao walishambulia kutoka sehemu tofauti hatua iliyowalazimu wanajeshi wa serikali kurudi nyuma kwenda mji wa Kunduz.
Ukosefu wa risasi na vikosi zaidi vilichangia kutekwa kwa wilaya ya Khanabad.
Taliban wamepiga hatua tangu vikosi vya kimataifa visitishe shughuli zao mwaka nchini Afghanistan 2014.
Wanajeshi wa Afghanistan kwa sasa wanapigana na wanamgambo hao walio karibu nusu ya wilaya zote 34 nchini humo
Mapema wiki hii Taliban walitaka wilaya moja iliyo mkoa jirani wa Baghlan.